Mwanaume mwenye kifafa afariki baada ya kuanguka juu ya makaa moto aliyokuwa anachoma Nakuru

, OCPD wa eneo hilo alisema kuwa uchunguzi zaidi umeanzishwa kubaini kilichotokea.

Muhtasari

•Alizirai na kuangukia makaa moto ambayo alikuwa anachoma katika kijiji kilicho kwenye mpaka wa kaunti ya  Nakuru na Narok.

crime scene
crime scene

Mwanaume mmoja  kutoka eneo ya Eburru, kaunti ya Nakuru alifariki dunia baada ya kuanguka juu ya makaa ambayo alikuwa anatayarisha.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 42 na ambaye ni mwathiriwa wa kifafa alizirai na kuangukia makaa moto ambayo alikuwa anachoma katika kijiji kilicho kwenye mpaka wa kaunti ya  Nakuru na Narok.

Alipokuwa anathibitisha tukio hilo, OCPD wa eneo hilo alisema  kuwa uchunguzi zaidi umeanzishwa kubaini kilichotokea.

"Mwanaume huyo alikuwa na kifafa na alikuwa anachoma makaa wakati alinguka kwenye moto na kuchomeka vibaya hadi akaaga" bosi wa polisi alisema.