Bangi na lita 107 za pombe haramu zapatikana Mlolongo

Muhtasari

•Shehena hiyo ambayo ilipatikana wakati wa msako uliofanywa katika eneo la Kapa, Syokimau ilikuwa pamoja na lita 77 za chang'aa, lita 30 za kangara, kilo 20 na misokoto 78 ya bangi.

•Hata hivyo hakuna yeyote aliyekamatwa kwani wenye shehena waliweza kutoroka baada ya kupata taarifa kuwa kulikuwa na msako ulikuwa unaendelea.

Madawa ya kulevya ambayo yalipatikana Mlolongo
Madawa ya kulevya ambayo yalipatikana Mlolongo
Image: CYRUS OMBATI

Zaidi ya lita 100 za pombe haramu na bangi zilipatikana maeneo ya Mlolongo kaunti ya Machakos siku ya Jumatano.

Shehena hiyo ambayo ilipatikana wakati wa msako uliofanywa katika eneo la Kapa, Syokimau ilikuwa pamoja na lita 77 za chang'aa, lita 30 za kangara, kilo 20 na misokoto 78 ya bangi.

Operesheni hiyo ilifanywa na naibu kamishna wa eneo la Mlolongo Dennis Ongaga, kamanda wa polisi katika kituo cha Syokimau Hamisi Chivasi, chifu wa Mlolongo Peter Ndunda, naibu chifu wa Syokimau David Kilonzo,naibu chifu wa Mlolongo Florence Kiio pamoja na maafisa wengine.

Hata hivyo hakuna yeyote aliyekamatwa kwani wenye shehena waliweza kutoroka baada ya kupata taarifa kuwa kulikuwa na msako ulikuwa unaendelea.

Naibu Kamishna Ongaga alisema kuwa shehena hiyo itaharibiwa iwapo hawataweza kukamata washukiwa.

Ongaga alisema kuwa ni ngumu kuweza kukamata yeyote katika eneo la Kapa kwani kuna pingamizi kubwa.