Jamaa anajisi mtoto wa miaka 5 na kumpatia shilingi 15 ili anyamaze kisha kutoweka Makueni

Muhtasari

•Musyoki alivizia mtoto huyo kwa njia kisha kumpeleka katika kichaka kilicho karibu ambako alimtendea unyama huo.

•Baada ya kutekeleza hayo jamaa huyo anasemekana kupatia mtoto yule shilingi kumi na tano ili aweze kubaki kimya kuhusiana na kilichokuwa kimetendeka.

crime scene
crime scene

Polisi  wanasaka jamaa mmoja anayedaiwa kutoweka baada ya kanajisi msichana wa miaka mitano katika kijiji cha Kilia, eneo la Mukaa, kaunti ya Makueni.

Peter Nzinzi Musyoki 40, anaripotiwa kutekeleza kitendo hicho cha unyama mnamo Jumatatu mida ya asubuhi wakati mtoto huyo alikuwa ametumwa kuchukua maziwa ya kutengezea kiamsha kinywa kwa jirani yao.

Kulingana na DCI, Musyoki alivizia mtoto huyo kwa njia kisha kumpeleka katika kichaka kilicho karibu ambako alimtendea unyama huo.

Baada ya kutekeleza hayo jamaa huyo anasemekana kupatia mtoto yule shilingi kumi na tano ili aweze kubaki kimya kuhusiana na kilichokuwa kimetendeka.

Hata hivyo, mama ya mhasiriwa ambaye alijawa na wasiwasi baada ya kuona bintiye alimkimbiza katika hospitali ya Kilungu Level 4 ambako alihudumiwa na ikathibitishwa kwamba alikuwa amenajisiwa.

Wapelelezi wametoa ombi kwa yeyote ambaye ana ripoti yeyote kuhusu aliko mshukiwa huku wakitia juhudi kumpata haraka iwezekanavyo.