Jamaa apiga mkewe risasi sita kufuatia mzozo wa mapenzi Nairobi

Muhtasari

•Baada ya kutekeleza unyama huo jamaa huyo anaripotiwa kukimbia eneo la tukio na kutoweka asijulikane aliko kufikia sasa.

crime scene 1
crime scene 1

Jamaa mmoja aliyeaminika kuua mkewe kufuatia mzozo wa mapenzi katika eneo la Mukuru jijini Nairobi anawindwa na polisi.

Wapenzi hao wanadaiwa kuzozana kwa kipindi kabla ya jamaa kutoa bastola yake na kumpiga mkewe risasi sita.

Baada ya kutekeleza unyama huo jamaa huyo anaripotiwa kukimbia eneo la tukio na kutoweka asijulikane aliko kufikia sasa.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti huku juhudi za kumsaka muuaji zikienedelea.