Jamaa wawili watiwa mbaroni kwa kushirikiana kubaka mwanamke mwenye ulemavu wa akili Lamu

Muhtasari

•Wawili hao walikuwa wameandamana na mzee wa nyumba kumi aliyetambulishwa kama Samuel Ngumi walipopata mwanamke mwenye ulemavu wa kiakili akitengeneza chai katika maeneo yasiyo salama.

•Ngumi alipigwa na butwaa kubwa aliporejea na kupata Murimi akijitosheleza kimapenzi na mwanadada yule mwenye umri wa wastani huku Kokane akiwa ashatoroka baada ya kumaliza zamu yake ya kukata kiu cha mapenzi na mwanamke yule.

crime scene
crime scene

Polisi katika kaunti ya Lamu wanazuilia jamaa wawili ambao wanadaiwa kushirikiana kubaka mwanamke mwenye ulemavu wa kiakili.

Shadrack Murimi 45 na Hiribae Kokane 43,  wanaripotiwa kubaka mwanamke huyo mida ya saa mbili usiku wa Jumatatu walipokuwa wanashika doria katika eneo la  Sina Mbio.

Kulingana na DCI, wawili hao walikuwa wameandamana na mzee wa nyumba kumi aliyetambulishwa kama Samuel Ngumi walipopata mwanamke mwenye ulemavu wa kiakili akitengeneza chai katika maeneo yasiyo salama.

Kufuatia hayo, mzee Ngumi alienda kutafutia mwanamke yule usaidizi na kuacha kama ameagiza washukiwa wabaki wakimlinda.

Ngumi alipigwa na butwaa kubwa aliporejea na kupata Murimi akijitosheleza kimapenzi na mwanadada yule mwenye umri wa wastani huku Kokane akiwa ashatoroka baada ya kumaliza zamu yake ya kukata kiu cha mapenzi na mwanamke yule.

Mzee Ngumi alisaidiana na wakazi kunusuru mwanamke huyo kisha kufahamisha polisi ambao waliwakamata jamaa wale na kuwatia korokoroni.

Mhasiriwa alipelekwa  kufanyiwa vipimo vya kidaktari katika zahanati ya Hindi Magogoni. Murimi na Kokane watafikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa ubakaji pindi wapelelezi watakamilisha uchunguzi wa.