DCI yamsaka mwanamume aliyemtupa mwanamke roshani Nyali

Muhtasari
  • DCI yamsaka mwanamume aliyemtupa mwanamke roshani Nyali
crime scene 1
crime scene 1

Msako umeanzishwa kwa mtu anayeshukiwa kumtupa mwanamke uchi nusu kutoka kwenye roshani ya chumba chao cha kulala katika vyumba vya  kulala vya Nyali's Sunny Side.

Mkurugenzi wa DCI George Kinoti alisema mtu huyo, Muyanga Suleiman, alimtupa mpenzi wake kwenye balcony saa tisa asubuhi Jumatatu.

"Mshukiwa anayeaminika kuwa raia wa kigeni alikimbia mara moja baada ya kufanya uhalifu," Kinoti alisema.

Kulingana na polisi, mlinzi katika nyumba hiyo alikuwa akifanya doria ufukweni, aliposikia mayowe ya mwanamke.

"Mlinzi alikaribia kwa uangalifu kile kilichoonekana kuwa kitu tu kugundua kwamba alikuwa mwanamke aliyekuwa uchi, ambaye alikuwa  amekufa na kulowa damu," alisema.

Mlinzi -Parsaoti Morinket - alikimbia kuelekea chumba cha msimamizi, ambapo alimjulisha tukio hilo.

"Walitembelea eneo la tukio na kudhibitisha kuwa mwili huo ulikuwa wa mwanamke wa miaka 25 ambaye alikuwa amealikwa mapema usiku kwenye chumba A10," alisema.

Walipokimbilia chumbani, walikuta mlango wake uko wazi na mtu huyo hayupo.

Wapelelezi wa eneo la Nyali walichanganua nyumba nzima kumtafuta mtuhumiwa lakini alikuwa tayari ametoweka.

Haya yanajiri siku chache baada ya wapenzi wawili kujitoa uhai, kwa kuruka kwenye gorofa kaunti ya Kilifi.