Vurugu za Kondele lazima zimemfurahisha Uhuru, Moses Kuria adai huku Mudavadi akizilaani vikali

Muhtasari
  • Katika mkutano huo, mbunge huyo alidai kuwa Uhuru alionekana kufurahia onyesho la vurugu huko Kibra na akaendelea kulifanyia mzaha
  • Wakati huo huo kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi alilaani vikali vurugu
Mbunge wa Gatunndu Kusini, Moses Kuria
Moses Kuria Mbunge wa Gatunndu Kusini, Moses Kuria
Image: Courtesy

Naibu Rais William Ruto, ambaye alikuwa katika siku yake ya pili ya ziara yake Nyanza, alikutana na wenyeji wa Kondele wenye chuki ambao waliupiga msafara wake kwa mawe.

Baada ya vurugu hivyo viongozi tofauti walionekana kutoa maoni tofauti huku Akitumia ukurasa wake wa Facebook mnamo Jumatano, Novemba 10, Kuria alirejelea machafuko yaliyotokea Kibra wakati wa uchaguzi mdogo wa 2019.

Katika mkutano huo, mbunge huyo alidai kuwa Uhuru alionekana kufurahia onyesho la vurugu huko Kibra na akaendelea kulifanyia mzaha.

Kuria alijuta kwamba alifikiria handshake kati ya Uhuru na kiongozi wa ODM Raila Odinga kulikusudiwa kufikia uvumilivu wa kisiasa na adabu kisiasa.

"Baada ya ghasia katika uchaguzi mdogo wa Kibra, tulikuwa na mkutano wa Mt Kenya huko Sagana. Rais Uhuru Kenyatta alionekana kufurahia kwa namna fulani onyesho la vurugu huko Kibra na kwa kweli aliifanyia mzaha

Handshake ilikuwa yote kuhusu utamaduni wa kuvumiliana na adabu ya kisiasa au hivyo tuliambiwa

Lakini nina uhakika popote alipo Uhuru Kenyatta, lazima atakuwa anacheka na kuwa na kishindo akitazama video kutoka Kondele," Aliandika KUria.

Wakati huo huo kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi alilaani vikali vurugu hivyo wakati wa mkutano wa naibu rais William Ruto.

“Inasikitisha kuona matukio ya vurugu yaliyotokea Kisumu leo. Tunapaswa kujifunza kuvumiliana katika nyanja zote za maisha. Vurugu huzaa ghasia zaidi jambo ambalo hatutaki," Mudavadi alisema.

Aliongeza kuwa, "Viongozi wote, IEBC, mashirika ya usalama, na Wakenya kwa jumla wanapaswa kukemea vitendo hivyo."