Mbunge wa Mvita awapoteza wafanyakazi 4 katika ajali mbaya ya barabarani

Muhtasari
  • Chama cha ODM kilithibitisha kisa hicho katika ujumbe wa Twitter kikisema wanne hao waliaga dunia Jumamosi jioni
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir
Image: Mkataba

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir amepoteza wanachama wanne wa timu yake kwenye ajali mbaya ya barabarani.

Chama cha ODM kilithibitisha kisa hicho katika ujumbe wa Twitter kikisema wanne hao waliaga dunia Jumamosi jioni.

Kulingana na ODM hao wanne walikuwa wafanyikazi wa Mbunge huyo. Kulingana na ripoti ya polisi, walifariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria kubingiria baada ya tairi kupasuka.

“Tunasikitika kupata taarifa ya kifo cha wanachama 4 wa timu ya Mh.Nassir ambao ni Ali Omar Naaman, Bi Carol Wayua Mueni, Athman Mohammed Omar na Elysian Musyoka kupitia ajali mbaya ya barabarani jioni ya leo. Tunaziombea familia za marehemu. wakati huu mgumu," taarifa ya ODM ilisoma.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu azidi kulaza roho zao mahal pema peponi.