Wanaume wanne taabani kwa kuvuka kwenye ardhi ya mwanasiasa mashuhuri Karen

Muhtasari
  • Wanaume wanne taabani kwa kuvuka kwenye ardhi ya mwanasiasa mashuhuri Karen
  • Ameiomba mahakama kutowazuilia washukiwa hao kama ilivyotakiwa na serikal
Image: Douglas Okiddy

HABARI NA ANNETTE WAMBULWA;

Washukiwa wanne wanaodaiwa kuingia katika ardhi ya kiongozi mashuhuri huko Karen wamefikishwa katika mahakama ya Milimani siku ya Jumatano.

Wanne hao ni Mohammed Muhammud Wako almaarufu Hussein Mohammed, James Owino Opere, Jonah Saluni Tuuko na Samakin Lesingiran.

Katika maombi tofauti ambayo yatawasilishwa mbele ya mahakama, serikali imekataa kufichua jina la kiongozi huyo ikisema ni kwa sababu za usalama.

"Kwa sababu ya maswala ya usalama, ningependa kutofichua jina lake," yasomeka maombi hayo mengine.

DCI inataka wanne hao kuzuiliwa kwa wiki moja katika kituo cha polisi cha Pangani ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi wao kuhusu madai ya uvunjaji sheria.

Polisi wanadai kuwa uchunguzi wa kisa hicho ni mgumu na utahitaji uchunguzi zaidi kufanywa ili kupata hati miliki ghushi.

“Baada ya kuhojiwa, kuna shaka ya kuamini kuwa washukiwa wanamiliki hati miliki ya kughushi ya ardhi hiyo wanayoitumia kuwarubuni wananchi wasio na hatia. kwa kuamini kwamba hatimiliki ni ya kweli na kwamba ardhi inatolewa kwa ajili ya kuuzwa” zinasomeka karatasi za mahakama.

Polisi pia wanataka kujua sababu ya madai ya kuingia kwa nguvu wakisema kuwa mali hiyo ni ya kiongozi huyo mashuhuri ambaye hakutajwa jina.

Wakili Danstan Omari anayewawakilisha James Opere na Jonah Saluni amepinga kuachiliwa kwao kwa dhamana.

Omari amemweleza Hakimu Mkazi Mkuu Jane Kamau kwamba wateja wake waliambiwa kuwa ardhi hiyo ni ya mkuu wa nchi.

" Wateja wangu wawili wameniambia kwamba waliambiwa kwamba ardhi ni ya mkuu wa nchi ndiyo maana wako hapa," Omari alisema.

Ameiomba mahakama kutowazuilia washukiwa hao kama ilivyotakiwa na serikali.

Upande wa mashtaka unasema kwa vile mmiliki halisi wa shamba hilo anafahamika wanamsaka Mmiliki huyo feki ambaye amekuwa akiwatapeli wananchi kwamba ardhi hiyo ni yake.

Jimbo linasema wanataka wanne hao kuwasaidia kumtafuta mmiliki anayedaiwa kuwa ghushi.

Omari aliiambia mahakama kuwa wateja wake walikuwa wakipita tu na hawakuvuka kama ilivyodaiwa.

Omari aliendelea kusema kwamba ardhi yote inayomilikiwa na Mkuu wa familia inalindwa na maafisa wa GSU kwa hivyo hakuna njia ambayo wangeweza kuivamia.

Hakimu Jane Kamau amesema hakuna sababu za msingi za kuwazuilia wanne hao kwa siku saba.

Hata hivyo amewaruhusu kuzuiliwa kwa siku bili, na kuachilia siku ya Ijumaa saa tano asubuhi, baada ya kutoa dhamana ya shilingi 30,000 kila mmoja