logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi JKIA wanamzuilia raia wa kigeni aliyepatikana na Sh110M za dola katika uwanja wa ndege

Alihojiwa na kuambia maafisa kwamba alifanya kazi Nairobi na alilipwa pesa taslimu.

image

Habari28 January 2022 - 13:00

Muhtasari


  • Khalid Jameel Saeed alikuwa amebeba pesa hizo kwenye mifuko kutoka Nairobi alipozuiwa alipokuwa akijaribu kupanda ndege ya Misri iliyokuwa ikielekea Manama

Raia wa Bahrain alizuiliwa Alhamisi usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta baada ya kupatikana akiwa amebeba angalau Sh107 milioni za dola za Marekani alipokuwa akijaribu kusafiri hadi nchini mwake.

Khalid Jameel Saeed alikuwa amebeba pesa hizo kwenye mifuko kutoka Nairobi alipozuiwa alipokuwa akijaribu kupanda ndege ya Misri iliyokuwa ikielekea Manama.

Maafisa katika uwanja huo wa ndege walisema kulingana na taarifa za kijasusi zilizoshirikiwa na Kituo cha Ripoti ya Fedha (FRC), wafanyikazi wa Mamlaka ya Ushuru wa Kenya (KRA) wa Udhibiti wa Mipaka katika Vituo vya Abiria vya JKIA walinasa abiria huyo wa kiume.

Alikuwa na nia ya kuabiria ndege hadi Bahrain kupitia Shirika la Ndege la Egypt na alikuwa amebeba USD 975,000 pesa taslimu ambayo ni takriban Sh110 milioni kwa kiwango cha ubadilishaji cha Sh113.

Tahadhari ilikuwa kwamba abiria huyo alikuwa amefanya majaribio kadhaa ya kuweka fedha katika benki lakini alishindwa.

Kisha akaamua kutembea na pesa hizo hadi kwenye kituo cha abiria katika harakati za kuondoka.

Alihojiwa na kuambia maafisa kwamba alifanya kazi Nairobi na alilipwa pesa taslimu.

Saeed aliachiliwa siku ya Ijumaa lakini pesa zake zilishikiliwa huku maafisa wakichunguza chanzo na nia yake. Polisi katika uwanja wa ndege walisema watatoa taarifa zaidi baadaye.

Maafisa wa KRA walisema suala hilo sasa linashughulikiwa na mashirika tofauti.

Maafisa katika uwanja wa ndege kwa kawaida hupata vitu vingi vya thamani kutoka kwa abiria wanaotaka kusafiri.

Thamani hizo ni pamoja na pesa taslimu na mapambo. Maafisa wanasema kuna haja ya mtu kutangaza kuhusu bidhaa hizo kabla hajasafiri.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved