Fahamu jinsi unavyoweza kusajili Simcard yako ya Safaricom mtandaoni bila kutembelea kituo

Muhtasari

•Siku ya Ijumaa, CA iliongeza muda wa makataa wa usajili wa simu kwa miezi sita hadi Oktoba 15, 2022.

Smart phone
Smart phone
Image: MAKTABA

Huku  Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) ikiwa imetoa amri kwa watumizi wa huduma za simu kusajili SimCards zao, Kampuni ya Safaricom imezindua njia ya kutekeleza shughuli hiyo mtandaoni.

Hii ni baada ya Wakenya kulalamika kwenye mitandao ya kijamii wakiomba kampuni hiyo kufuata nyayo za Telkom ambao tayari walikuwa wameanzisha usajili wa Sim Card mtandaoni.

Siku za hivi majuzi foleni ndefu zimeshuhudiwa katika vituo  mbalimbali vya usajili wa laini kote nchini huku Wakenya wakiwa mbioni kuepuka kufungiwa.

Siku ya Ijumaa, CA iliongeza muda wa makataa wa usajili wa simu kwa miezi sita hadi Oktoba 15, 2022.

Watumizi wa simu ambao hawatakuwa wamesajili laini zao kufikia Oktoba 15 wanahatarisha kufungiwa laini zao.

Ili kusajili laini yako mtandaoni, fuata maelezo yaliyo kwenye link hii>>>