BURIANI KIBAKI:Hii hapa ratiba kamili ya mazishi ya hayati Mwai Kibaki

Muhtasari
  • Askofu mkuu Anthony Muheria huenda akaongoza ibada hiyo ikizingatiwa kuwa ni eneo lake la mamlaka
Misa ya Hayati Mwai Kibaki yaendelea katika uwanja wa Nyayo mnamo Aprili 29,2022
Misa ya Hayati Mwai Kibaki yaendelea katika uwanja wa Nyayo mnamo Aprili 29,2022
Image: EZEKIEL AMINGA

Mwili wa marehemu Rais Emilio Mwai Kibaki utaondoka katika Makao ya Mazishi ya Lee saa saba kamili asubuhi na unatarajiwa kuwasili Othaya, Kaunti ya Nyeri kufikia saa nne asubuhi

Mwili huo utasafirishwa kwa barabara kulingana na matakwa ya Kibaki.

Ibada ya mazishi ya Kibaki itaanza saa 10 asubuhi hadi saa saba mchana.

Ibada itaongozwa na kanisa katoliki.

Askofu mkuu Anthony Muheria huenda akaongoza ibada hiyo ikizingatiwa kuwa ni eneo lake la mamlaka.

Kati ya saa nne  asubuhi hadi saa saba mchana  kanisa katoliki litaongoza misa takatifu ambayo itajumuisha maombi kwa familia, sifa za mwisho za baraka na heshima.

Kuanzia saatisa jioni hadi saa kumi usiku, hafla ya kumwombea itafanyika ambayo itajumuisha ibada ya mwisho kwenye kaburi, maandamano ya mazishi ya serikali, heshima za kijeshi zilizokamilika kwa salamu 19 za bunduki, sala ya kujitolea, sala, heshima ya muziki na heshima ya maua.

Salamu hiyo ya bunduki ni kwa heshima ya jukumu lake kama jenerali nyota tano na kamanda mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Kenya.

Baada ya mwili huo kushushwa kaburini, Rais Uhuru Kenyatta ataongoza kimya cha dakika moja kwa heshima ya marehemu.

Hatazikwa na bendera ya Taifa. Bendera itakabidhiwa kwa familia baada ya kulazwa.

Haya yote yatafanyika nyumbani kwa rais Othaya