Mbwa wawaua mama na mwanawe Ugenya

Muhtasari
  • Akithibitisha kisa hicho, naibu OCPD wa Ugenya James Ngao alisema kuwa Caren Akinyi Aluoch mwenye umri wa miaka 28 aliuawa pamoja na mtoto wake wa kiume wa mwaka mmoja
Mbwa waliofungiwa kwa ajili ya kuchinjwa huko Korea
Mbwa waliofungiwa kwa ajili ya kuchinjwa huko Korea
Image: COEXISTENCE OF ANIMAL RIGHTS ON EARTH (CARE)

Mama na mwana wameuawa na mbwa katika eneo la Simur, Kaunti Ndogo ya Ugenya.

Mbwa hao walifugwa katika boma moja eneo la Siranga.

Kulingana na meneja wa nyumba hiyo, mbwa hao wakali walikuwa wametoroka kutoka kwenye banda lao Jumapili usiku na majaribio ya kuwatafuta hayakufaulu.

Akithibitisha kisa hicho, naibu OCPD wa Ugenya James Ngao alisema kuwa Caren Akinyi Aluoch mwenye umri wa miaka 28 aliuawa pamoja na mtoto wake wa kiume wa mwaka mmoja.

"Msimamizi wa nyumba aliripoti kwamba mbwa walikuwa wametoka nje ya boma. Mwanamke huyo na mtoto wake walipatikana Jumatatu asubuhi wakiwa wamepasuliwa na mbwa hao wakatili,” Ngao alisema.

Wenyeji waliwapiga mbwa hadi kufa.

Miili ya bibi huyo na mwanawe imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha kaunti ndogo ya Ukwala.