Sababu ya kufika mbele ya jopo la Azimio-Kalonzo Musyoka

Muhtasari
  • Kalonzo sasa atasubiri jopo kuamua ni nani anafaa kuwa mgombea mwenza wa Raila
KINARA WA WIPER KALONZO MUSYOKA
Image: ENOS TECHE

Kwa muda wa siku chache zilizopita kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amekuwa akijipiga kifua hangefika mbele ya jopo la Azimio.

Kulingana na Kalonzo mwaliko huo unadhalilisha na alikuwa akichagua mazungumzo na rais Uhuru kenyatta na mshirika wake Raila Odinga.

Hata hivyo akizungumza na wanahabari Kalonzo Musyoka, amefichua sababu iliyomfanya kuhudhuria mahojiano hayo huku akitoa maelezo ya kilichotokea ndani.

"Yalikuwa mazungumzo, si mahojiano. Niliamua kufika mbele ya jopo la Azimio kwa sababu hatukutaka kumpa mtu yeyote kisingizio cha kusema, 'aligomea kuja.' Yalikuwa mazungumzo ya ajabu.

Kalonzo sasa atasubiri jopo kuamua ni nani anafaa kuwa mgombea mwenza wa Raila.

Kalonzo alikuwa ameahidi kuondoka katika muungano huo iwapo wangemnyima nafasi ya naibu wa Raila akisema ndiye mgombeaji aliyefuzu zaidi hadi sasa.

“Kamati ina wanaume wakubwa na wazoefu kama Askofu Njenga na Askofu Zacheus Okoth, nililitazama hilo kivyangu na kusema kwa nini sitaki kwenda kukutana na Askofu Okoth? Ilibidi nifanye uamuzi huo.”