Uhuru, Ruto wakutana katika kikao cha baraza la mawaziri Ikulu

Muhtasari
  • Haya yanajiri baada ya Naibu Rais Ruto kudai kuwa hakuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri baada ya majukumu yake kudaiwa kukabidhiwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto walikutana Alhamisi kwa mkutano wa Baraza la Mawaziri.

Wawili hao walikutana katika Ikulu ya Nairobi, ambapo mkuu wa nchi ndiye anaongoza mkutano huo kwa sasa.

Taarifa kutoka Ikulu ilisema masuala ya umuhimu ya kitaifa na kimataifa yatajadiliwa wakati wa mkutano huo.

"Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta leo yuko Ikulu, Nairobi, akiongoza kikao kamili cha Baraza la Mawaziri ambapo masuala kadhaa ya umuhimu wa kitaifa na kimataifa yatajadiliwa."

Haya yanajiri baada ya Naibu Rais Ruto kudai kuwa hakuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri baada ya majukumu yake kudaiwa kukabidhiwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i.

Ruto amekosekana katika mikutano ya awali ya Baraza la Mawaziri.