Polisi wanamsaka mwanamume anayeshukiwa kumuua bintiye Kajiado

Muhtasari
  • Polisi wanamsaka mwanamume anayeshukiwa kumuua bintiye Kajiado
Crime Scene

Polisi wanamsaka mwanamume ambaye yuko mafichoni baada ya kudaiwa kumuua bintiye wa umri wa miaka 11 na kumjeruhi mwanawe siku ya Jumamosi.

Kulingana na msimamizi wa kijiji Willy Kalovya, mwanamume huyo wa umri wa makamo alitoroka baada ya kisa hicho katika kijiji cha Kilungu B katika Kaunti Ndogo ya Kibwezi, Kaunti ya Makueni mwendo wa saa sita usiku.

Kalovya alisema mshukiwa alikuwa akiishi na familia yake katika Kaunti ya Kajiado na alikuwa amefika Jumamosi nyumbani kwake kijijini na watoto wake wawili. Aliongeza kuwa mshukiwa huyo amekuwa na tofauti za ndoa na mkewe, jambo ambalo lilisababisha hali hiyo mbaya.

Mvulana aliyejeruhiwa tangu wakati huo amekimbizwa katika hospitali ya Kaunti Ndogo ya Kibwezi kwa matibabu.