Hisia mseto baada ya Sankok kutangaza kustaafu kutoka kwa siasa

Muhtasari
  • Hisia mseto baada ya Sankok kutangaza kustaafu kutoka kwa siasa
MBUNNGE MTEULE SANKOK
Image: RADIOJAMBO

Mbunge mteule David Sankok Jumatatu alitangaza kuwa anastaafu kutoka kwa siasa,huku akiibua hisia mseto mitandaoni.

Akizungumza katika mahojiano katika Spice FM, Sankok alisema hatafuti kiti chochote cha kuchaguliwa katika uchaguzi ujao wa Agosti kwani anataka kuangazia biashara za kibinafsi.

“Suala la kugombea ni uamuzi wa mtu binafsi. Niliamua wakati huu kutotafuta nafasi yoyote ya kuchaguliwa. Ninahitaji kuzingatia biashara zangu," alisema.

Alibainisha kuwa alianza kupigania haki za watu wanaoishi na ulemavu akiwa na umri mdogo na hakuwahi kupata nafasi ya kukuza biashara zake.

Sankok, mfuasi wa UDA, alipanda jukwaani kuunga mkono manifesto ya Naibu Rais William Ruto, akiwahimiza Wakenya kupiga kura kwa busara katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.

Sankok alisema hapo awali kuwa tangu kuteuliwa kwake katika Bunge la Kitaifa mwaka wa 2017, siasa zimemletea hasara kubwa ya kifedha.

Habari za kustaafu kwake ziliibua hisia mseto mitandaoni.