DP Ruto amuomboleza mwigizaji wa filamu Nairobi Half Life Olwenya Maina

Olwenya pia alifanya kazi kama msanii wa sauti katika matangazo mbalimbali.

Muhtasari
  • Katika ujumbe wake wa rambirambi, DP alimkumbuka Olwenya kama mwigizaji mahiri ambaye ametoka jukwaani hivi karibuni
OLWENYA MAINA
Image: KWA HISANI

Naibu Rais William Ruto ameomboleza mwigizaji Maina Olwenya aliyeaga dunia Jumatatu usiku baada ya kuzirai.

Katika ujumbe wake wa rambirambi, DP alimkumbuka Olwenya kama mwigizaji mahiri ambaye ametoka jukwaani hivi karibuni.

"Ninaomboleza pamoja na familia, marafiki na wafanyakazi wenzangu. Tumepoteza talanta ya kweli, mbunifu aliyejitolea na mtu mzuri. Kama vile talanta zote kuu, Maina ataendelea na kazi yake. Safiri Salama," Ruto alisema.

Olwenya, ambaye aliigiza Oti katika filamu ya Nairobi Half Life 2012, alitangazwa kuwa amefariki katika hospitali ya Nairobi ambapo alikimbizwa baada ya kuzirai.

Chanzo cha kifo bado hakijajulikana lakini familia hiyo, ambayo imetaka kuwepo kwa utulivu na faragha wakati huu, itatoa taarifa zaidi ikiwa tayari.

Wakati huo huo, uchunguzi kuhusu kifo cha ghafla cha Olwenya umeanza.

Olwenya pia alifanya kazi kama msanii wa sauti katika matangazo mbalimbali.

PIa amewahi fanya matangazo kwenye Radiojambo.