logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Marekani haina taarifa za kupendekeza hali ya usalama Kisumu-Gavana Anyang' Nyong'o

Gavana huyo alikuwa akijibu ushauri wa usafiri uliotolewa Jumanne, Agosti 2 na Ubalozi wa Marekani

image
na Radio Jambo

Makala03 August 2022 - 17:35

Muhtasari


  • Ubalozi pia uliwashauri raia wake kuwa waangalifu dhidi ya maandamano au mikutano yoyote inayohusiana na uchaguzi kwani inaweza kugeuka kuwa ya vurugu
Magavana James Ongwae (Kisii), Anyang' Nyong'o (Kisumu) na Abdi Mohamud (Wajir) wakihutubia wanahabari nje ya afisi za Baraza la Magavana huko Oracle, Westlands, Aprili 1. Picha: MAKTABA

Gavana wa Kisumu Profesa Anyang' Nyong'o amewataka raia wa Marekani na watalii wengine au wawekezaji wanaotarajiwa kutembelea jiji la tatu kwa ukubwa nchini Kenya kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9. .

Gavana huyo alikuwa akijibu ushauri wa usafiri uliotolewa Jumanne, Agosti 2 na Ubalozi wa Marekani nchini Kenya, ukisema kwamba walikuwa wameweka vizuizi vya kusafiri kwa wafanyikazi huko Kisumu.

Profesa Nyong'o alipokuwa akihutubia wanahabari aliwahakikishia wageni wanaotarajiwa kuwa jiji liko salama na kuwataka wote kutembelea jiji la machweo.

"Ninataka kuwahakikishia wanaosafiri kwenda Kisumu kwamba watu wetu ni watulivu na wanatarajia kuwakaribisha. Furahia jiji letu zuri la machweo," alisema.

Kulingana na ubalozi huo, mara kwa mara Kenya imekuwa na vurugu za kabla ya uchaguzi wakati wa mizunguko ya uchaguzi. Kwa hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje imewakumbusha raia wake wa U.S juu ya hitaji endelevu la kuwa waangalifu.

Ubalozi pia uliwashauri raia wake kuwa waangalifu dhidi ya maandamano au mikutano yoyote inayohusiana na uchaguzi kwani inaweza kugeuka kuwa ya vurugu.

"Maandamano mara kwa mara yanaweza kuwa ya vurugu, yakihitaji kuingilia kati kwa polisi. Migomo na shughuli nyingine za maandamano zinazohusiana na hali ya kiuchumi hutokea mara kwa mara," ilisoma taarifa kwa sehemu.

Hata hivyo, gavana huyo alielezea kutokubaliana kwake na ushauri huo, akitumia fursa hiyo kukumbusha Ubalozi wa Marekani, Kisumu hivi majuzi uliandaa Kongamano la Africities ambapo wageni kutoka kote ulimwenguni walihudhuria.

Kupitia kwenye taarifa Gavana huyo alisema kwamba Marekani haina taarifa yeyote ya kutoa kuhusu usalama wa Kisumu au nchini Kenya.

Aidha kiongoozi huyo aliweka wazi kwamba kutakuwa na usalama kabla,wakati na baada ya uchaguzi.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved