Uhuru na mimi ni ndugu milele - Mtoto wa Museveni Muhoozi

Akizungumzia mkutano huo, Muhoozi alimwita tena Uhuru ndugu yake, akimtaja kama shujaa mkuu.

Muhtasari
  • Hii si mara ya kwanza kwa Muhoozi kutangaza urafiki wake na rais
  • Baada ya mkutano naye katika Ikulu ya Nairobi mnamo Juni 18, Muhoozi aliandika
Muhoozi Kainerugaba na Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni Muhoozi Kainerugaba bado amesisitiza urafiki wake na Rais Uhuru Kenyatta.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter, Muhoozi alisema rais anayeondoka atabaki kuwa rafiki yake milele.

"Mimi na Rais Uhuru ni ndugu milele!" alitweet siku ya Jumatano.

Hii si mara ya kwanza kwa Muhoozi kutangaza urafiki wake na rais.

Baada ya mkutano naye katika Ikulu ya Nairobi mnamo Juni 18, Muhoozi aliandika

"Sisi ni ndugu milele. Mimi na kaka yangu mkubwa H.E Uhuru Kenyatta."

Muhoozi alikuwa amemtembelea Rais Uhuru katika Ikulu ya Nairobi, ambako walijadili masuala ya pande mbili na ya kimataifa yenye maslahi kwa nchi zote mbili.

Akizungumzia mkutano huo, Muhoozi alimwita tena Uhuru ndugu yake, akimtaja kama shujaa mkuu.

"Ilikuwa heshima na furaha kukutana na kaka yangu mkubwa na rafiki Rais Uhuru Kenyatta jijini Nairobi hivi majuzi. Pia nilimpelekea ujumbe maalum kutoka kwa H.E. Kaguta Museveni," alisema.

"Baada ya kukutana na kaka yangu mkubwa Nairobi, H.E. Uhuru, Mwenyekiti wetu wa EAC, naamini tuna njia ya amani Mashariki mwa DRC. Wapiganaji wakubwa ni wale wanaotafuta amani juu ya vita!"