KEMSA yaahidi kuimarisha usambazaji vifaa vya matibabu katika kaunti

Alisema halmashauri ya KEMSA imetoa dawa za thamani ya shilingi bilioni 27 kote nchini wakati wa mwaka uliopita wa kifedha.

Muhtasari
  • Ramadhani amesema halmashauri hiyo inalenga kukusanya angalau shilingi milioni 500 kila mwezi kutoka serikali za kaunti ili kuboresha utoaji huduma
Afisa mkuu mtendaji wa halmashauri ya KEMSA Terry Ramadhani na gavana mteule nathif Adam
Image: KEMSA/TWITTER

Halmashauri ya usambazaji dawa hapa nchini (KEMSA) imeahidi kusaidia ajenda ya kuhimiza afya njema katika kiwango cha kaunti ya magavana wapya kama shemu ya mkakati wa mageuzi wa halmashauri hiyo.

Akiwa na wa gavana mteule wa kaunti ya Garissa Nathif Jama, siku ya Alhamisi afisini mwake , afisa mkuu mtendaji wa halmashauri ya KEMSA Terry Ramadhani, alisema serikali za kaunti ni wateja wa halmashauri hiyo na kwamba halmashauri hiyo inafanya kila juhudi katika kuhakikisha wanatimiza awamu ya mwisho ya mahitaji ya usambazaji dawa.

Alisema halmashauri ya KEMSA imetoa dawa za thamani ya shilingi bilioni 27 kote nchini wakati wa mwaka uliopita wa kifedha.

Ramadhani amesema halmashauri hiyo inalenga kukusanya angalau shilingi milioni 500 kila mwezi kutoka serikali za kaunti ili kuboresha utoaji huduma.