Urusi Yampongeza Rais Mteule Ruto kwa Ushindi

Urusi imejiunga na mataifa mengine kumpongeza rais mteule wa Kenya William Ruto kwa kuteuliwa kama rais wa tano wa Kenya.

Muhtasari

• "Tuna Imani kwamba urafiki baina yetu utaendelea kati ya mataifa haya mawili na watu wake na utazidi kuboreshwa na kudumishwa,”

Rais wa Urusi Vladmir Putin na rais mteule wa Kenya William Ruto
Rais wa Urusi Vladmir Putin na rais mteule wa Kenya William Ruto
Image: MAKTABA
Rais wa Urusi Vladmir Putin na rais mteule wa Kenya William Ruto
Rais wa Urusi Vladmir Putin na rais mteule wa Kenya William Ruto
Image: MAKTABA

Tangu rais mteule William Ruto atangazwe rasmi na tume ya IEBC kuwa mrithi wa rais Uhuru Kenyatta, viongozi mbalimbali kote uliwenguni wameendelea kutuma pongezi zake kwa ushindi wake.

Hongera za hivi karibuni ni kutoka kwa ubalozi wa Urusi jijini Nairobi ambapo kama ni kweli kulingana na waraka unaoenezwa kweney mitaandao ya kijamii, inaonesha imetoka katika ubalozi wa Urusi ukimpongeza raia mteule Ruto kwa ushindi wake.

“Ubalozi wa taifa la Urusi nchini Kenya unajivunia kumhongera mheshimiwa William Ruto kutokana na kutangazwa kwake kama rais mteule wa Kenya. Urusi inatazamia kuendeleza uhusiano wake na Kenya. Tuna Imani kwamba urafiki baina yetu utaendelea kati ya mataifa haya mawili na watu wake na utazidi kuboreshwa na kudumishwa,” waraka huo ulioibuliwa kwenye mitandao ulisoma.

Hongera hizi zinakuja siku mbili tu baada ya kinara wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga kujitokeza wazi na kupuuzilia mbali matokeo hayo yaliyomuweka Ruto mshindi na kudokeza kwamba timu yake itaelekea mahakamani kuyapinga rasmi kisheria.