Rais Uhuru Kenyatta awashukuru Wakenya kwa kuunga mkono serikali yake

Wakati akitoa hotuba yake ya kuaga, Uhuru alitoa shukrani zake kwao kwa kumuunga mkono.

Muhtasari
  • Akizungumza siku ya Ijumaa katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex, Uhuru aliwataka kusalia imara katika utawala unaokuja
Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta amewaambia Wanajeshi wa Ulinzi wa Kenya kuunga mkono utawala unaokuja kama walivyomfanyia.

Akizungumza siku ya Ijumaa katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex, Uhuru aliwataka kusalia imara katika utawala unaokuja

“Nawasalimu kila mmoja wenu kwa kujitolea kwenu kwa wajibu. Ninawaomba muwe imara katika utawala unaokuja kama vile mlivyounga mkono utawala wangu na wa watangulizi wangu,” alisema.

"Nitawapeza lakini bado tuko pamoja."

Wakati akitoa hotuba yake ya kuaga, Uhuru alitoa shukrani zake kwao kwa kumuunga mkono.

"Ninashukuru ushiriki ambao KDF imetoa sio tu katika sekta ya usalama lakini pia katika maendeleo ya taifa letu," alisema.

 

Uhuru pia aliwataka wanajeshi wa KDF na waliokuwepo kwenye hafla hiyo kuzingatia muda wa kimya kwa heshima ya Malkia Elizabeth II, aliyefariki siku ya Alhamisi.

Rais alisema viongozi wasio na uwezo na usimamizi mbaya umemsukuma kusajili uongozi wa kijeshi katika mashirika.

Uhuru aliwashukuru Wakenya wote kwa kumuunga mkono katika kipindi chake cha miaka 10.

"Ninawashukuru Wakenya kwa dhati kwa msaada wa ajabu ambao ulitoa mchango mkubwa katika ustawi wa taifa letu," alisema.