Tumefikia usawa wa kijinsia jeshini - Uhuru

Alisema wako katika jitihada za kufikia uwezeshaji wa wanawake katika utawala.

Muhtasari
  • Alisema wanawake ni nguzo ya jamii yoyote inayotaka kufanikiwa
  • Uhuru alisema sera za usawa wa kijinsia pia ziliimarishwa katika idara na wizara zingine za serikali
Rais anayeondoka Kenyatta amesema kiongozi wake ni Raila
Rais anayeondoka Kenyatta amesema kiongozi wake ni Raila
Image: State House Kenya

Rais Uhuru Kenyatta amesema nchi iliweza kufikia usawa wa kijinsia katika utawala wa kijeshi wakati wa uongozi wake.

Akitoa hotuba yake ya kuaga siku ya Ijumaa katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex huko Lang'ata, Uhuru alisema sera za usawa wa kijinsia pia ziliimarishwa katika idara na wizara zingine za serikali.

Alisema wako katika jitihada za kufikia uwezeshaji wa wanawake katika utawala.

"Katika miaka 10 iliyopita, utawala wangu ulipitisha mipango ambayo iliifanya Kenya kuchipua sababu ya kufikia usawa wa kijinsia," alisema.

Alisema wanawake ni nguzo ya jamii yoyote inayotaka kufanikiwa.

"Wana uwezo wa kushawishi mabadiliko chanya," aliongeza.

Uhuru aliwataja Balozi Raychelle Omamo na Monica Juma ambao wamehudumu kama makatibu wa baraza la mawaziri katika Wizara ya Ulinzi.

Omamo, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa sasa alihudumu kama Waziri wa Ulinzi kuanzia Mei 15, 2013, hadi Januari 14, 2020.

Juma alihudumu kama Waziri wa Ulinzi kuanzia Januari 14, 2020 hadi Septemba 30, 2021.

Pia alidokeza kuwa utawala wake uliona kuteuliwa kwa Fatuma Ahmed kama Meja Jenerali wa kwanza wa kike wa Jeshi la Kenya.

Meja Jenerali Ahmed aliteuliwa mnamo Julai 14, 2018.

“Ninaamini yote haya ni maendeleo kuelekea kuhusisha na kuhakikisha kuwa jinsia inazingatiwa katika sera zote na katika nyanja zote za utawala,” Uhuru alisema.

Katika kumuenzi Uhuru, Jenerali wa KDF Robert Kibochi alisema kumbukumbu za Rais anayeondoka zitasalia kwa wanajeshi.

"Umeacha nyuma moja ya taasisi bora za kijeshi barani," alisema.