logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Junet hakula hata senti ya pesa za maajenti - Kamati ya kampeni za Odinga

"Junet hakuwahi hata mara moja kushughulikia fedha zilizokusudiwa kwa mawakala - Makau Mutua

image
na Radio Jambo

Habari11 September 2022 - 11:20

Muhtasari


• Bw Mohammed hakuwa na uhusiano wowote na usimamizi wa mawakala,” alisema Prof Mutua.

Junet Mohammed wakinong'onezeana na Odinga

Baada ya kupoteza uchaguzi wa urais na pia kesi katika ombi la kutaka matokeo kutupiliwa mbali, sasa mzozo ndani ya muungano pana zaidi wa kisiasa nchini Azimio la Umoja One Kenya unazidi kutokota hata zaidi.

Baadhi ya viongozi ndani ya muungano huo wameanza kufanya marejeleo ya kutafuta kiini cha kiongozi wao Raila Odinga kupoteza kwa mara ya tano mfululizo, haswa kipindi hiki amabcho alikuwa amepewa kipaumbele na kura za maoni kuibuka mshindi.

Marejeleo haya yameibua lawama zikitupwa kushoto kulia kwa wanasiasa waliokuwa karibu na Odinga. Mbunge wa Suna East Junet Mohammed amekuwa mwanasiasa wa hivi karibuni kuangukiwa na tope la lawama ambapo baadhi ya watu ndani ya Azimio wamesema alichangia kuanguka kwa Raila kwa kula pesa za maajenti na za kampeni.

Huku Junet aakizidi kuandamwa na lawama na kkashfa kama hizo, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya kampeni za Odinga, msomi Makau Mutua amejitokeza kimasomaso kumtetea Junet kwa kusema kwamba hakuhusika hata kidogo na pesa hizo na wala hakuzipunja.

“Nimeona mashambulizi ya kihuni dhidi ya Junet Mohammed yakimtuhumu kwa ufujaji wa pesa zilizokusudiwa kwa mawakala. Acha niseme bila ubishi kwamba Bw Mohammed alikuwa kinara wa kampeni katika uwanja huo akimuunga mkono Raila Odinga. Hakuwahi hata mara moja kushughulikia fedha zilizokusudiwa kwa mawakala. Wala Bw Mohammed hakuwa na uhusiano wowote na usimamizi wa mawakala,” alisema Prof Mutua.

Mutua alizidi kusema katika barua hiyo kwamba hakuna mtu yeyote ndani ya Azimio anafaa kubebeshwa lawama za kupoteza kwa uchaguzi wa urais kwa sababu kila mtu alicheza katika nafasi yake k ikamilifu na uchaguzi ulihitilafiwa na tume ye IEBC yenyewe.

“Muhimu, niseme wazi kwamba suala la mawakala halikuwa sababu ya uchaguzi kuhitilafiwa. Hakuna anayepaswa kulaumiwa Azimio au wagombeaji wetu kwa kura zilizoibiwa au uchaguzi ambao ulikuwa na dosari mbaya,” Prof Mutua alilainisha mambo.

Lawama ndani ya muungano huo zinatishia mfumuko haat zaidi, jambo ambalo limetajwa kuwa athari kubwa katika kuendesha shughuli za upinzani kikamilifu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved