Gachagua atembelea timu ya msafara wa rais waliojeruhiwa kwenye ajali

Taarifa za ajali ya barabarani bado ni chache

Muhtasari

• Tarehe na chanzo cha ajali bado hakijajulikana.
• Mnamo Jumatatu, Gachagua alichukua afisi ya Harambee Annex ambayo awali ilikuwa inakaliwa na Rais William Ruto.

DP Gachagua amtembelea afisa wa Msindikizaji wa Rais katika Hspital
DP Gachagua amtembelea afisa wa Msindikizaji wa Rais katika Hspital
Image: THE STAR

Naibu Rais Rigathi Gachagua amefichua kuwa kulikuwa na ajali iliyomhusisha afisa wa kumsindikiza rais iliyompelekea kulazwa hospitalini.

"Ilichukua muda kuwatembelea maafisa wa kumlinda rais waliolazwa hospitalini baada ya ajali ya barabarani," alisema. Tarehe na chanzo cha ajali bado hakijajulikana.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Naibu rais alisema kuwa afisa huyo ataachiliwa siku chache zijazo kufuatia mazungumzo na daktari wake. "Nina furaha wamepata maendeleo makubwa na madaktari walinihakikishia kuachiliwa siku chache zijazo. Tunawapongeza maafisa wetu wa polisi kwa uzalendo na kujitolea kwao."

Mnamo Jumatatu, Gachagua alichukua katika afisi ya Harambee Annex ambayo awali ilikuwa inakaliwa na Rais William Ruto.

 

Ruto alihudumu kama Naibu Rais kwa miaka 10 kabla ya kuchaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa Agosti 9. Rais sasa atahamia Harambee House ambako ofisi yake ina makao yake.

Katika taarifa baada ya kukaa ofisini, Gachagua alisema yuko tayari kutekeleza jukumu lake kama wa pili katika uongozi. "Sasa tuko tayari kufanya kazi na kubadilisha mwelekeo wa nchi yetu kuelekea ahueni. Nimetulia katika afisi yangu mpya ya Harambee House Annex na mifumo yote inakwenda," alisema.