Migori: Majambazi watatu watiwa mbaroni kufuatia visa vya mauaji

Watatu hao wanahusishwa na kifo cha mtu mmoja aliyepatikana ameuawa na majeraha mabaya shingoni.

Muhtasari

• Hiki si kisa cha kwanza kuripotiwa eneo hili kwani mwezi huu, mwili wa mtu mmoja ulipatikana ukiwa umetupwa barabarani ukiwa na majeraha shingoni.

Pingu
Image: Radio Jambo

Polisi eneo la Suna Mashariki kaunti ya Migori wamewakamata washukiwa watatu wanaoaminika kuwa miongoni mwa genge ambalo limekuwa likiwahangaisha wakaazi.

Msaidizi wa Chifu wa Nyabisawa, Barack Ogaja alisema watatu hao walitiwa mbaroni katika msako unaoendelea kuwalenga wale waliohusika na msururu wa uvunjaji.

 "Washukiwa walikamatwa muda mfupi baada ya kuvunja duka katika kituo cha biashara cha Nyamanga," Chifu Ogaja alisema.

Washukiwa hao wanashikiliwa na polisi katika harakati za kuwatafuta walioshirikiana nao, kufuatia msururu wa visa vya wizi. Wananchi wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na polisi ili kuwakamata wahusika wote.

Hiki si kisa cha kwanza kuripotiwa eneo hili kwani mwezi huu, mwili wa mtu mmoja ulipatikana ukiwa umetupwa barabarani ukiwa na majeraha shingoni eneo la Forodha huko Nyabomo, Kaunti Ndogo ya Nyatike.

Ongezeko la magenge hawa ni jambo linalo wafanya wakaazi wa mogori kuirai serikali iwahakikishie usalama ndivyo waishi bila woga wowote.