Wavinya Ndeti, akizindua vifaa hivyo alibainisha kuwa hii ilikuwa sehemu ya mpango wake wa siku 100 wa matokeo ya haraka ili kuboresha kikamilifu sekta ya afya katika kaunti hiyo.

Machakos. Vituo vya afya vyapokea nyongeza ya dawa na vifaa vya matibabu

Aidha alibainisha kuwa kaunti hiyo inajitahidi kuzindua mpango wa Afya bila malipo kwa wazee na walemavu katika jamii hivyo wasiokuwa kwenye bima iyo wajiandikishe.

Muhtasari

"Pia naomba wale wote ambao hawako kwenye mpango wa afya, tafadhali, wajiandikishe.," Gavana alisema.

Wavinya ndeti kati ya mbinu zake za siku 100 ni kuboresha matibabu.
Wavinya ndeti kati ya mbinu zake za siku 100 ni kuboresha matibabu.

Vituo vya matibabu vya kaunti ya Machakos vimepokea nyongeza ya dawa na vifaa vya matibabu vya thamani ya shilingi milioni 50 kutoka kwa Wakala wa KEMSA na wauzaji wengine.

Gavana wa Kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti, akizindua vifaa hivyo alibainisha kuwa hii ilikuwa sehemu ya mpango wake wa siku 100 wa matokeo ya haraka ili kuboresha kikamilifu sekta ya afya katika kaunti hiyo.

Wavinya hata hivyo alionya mashirika katika hospitali zinazohusika na uuzaji wa dawa, kwamba siku zao zimehesabiwa huku akitoa wito wa uwajibikaji mkali.

"Wasimamizi wote wanaosimamia usambazaji lazima wawajibike kupokea, kutumia na usalama wa vifaa," Wavinya alisema.

Wakati uo huo, gavana aliyekuwa Katibu Mkuu kwenye utawala wa uchukuzi na miundombinu, alitoa wito kwa wakaazi hao kujiandikisha katika mpango wa Bima ya afya ili kurahisisha huduma zao za afya katika kaunti hiyo.

Aidha alibainisha kuwa kaunti hiyo inajitahidi kuzindua mpango wa Afya bila malipo kwa wazee na walemavu katika jamii hivyo wasiokuwa kwenye bima iyo wajiandikishe.

"Pia naomba wale wote ambao hawako kwenye mpango wa afya, tafadhali, wajiandikishe. Tunashughulikia njia za kuona ikiwa tunaweza kuhudumia walemavu na wale walio na umri wa zaidi ya miaka 65, wajiandikishe," Gavana aliongezea.