Dubai yaandaa maonyesho ya utalii Kenya, Uganda na Ethiopia

Roadshow ya Kenya itafanyika Septemba 22.

Muhtasari

• Maonyesho hayo yataangazia ziara za bei nafuu jijini Dubai na huduma zingine  jiji hilo kwa washirika wake muhimu wa usafiri katika miji inayolengwa.

• Vivutio vya onyesho hayo ni katika sekta za safari, ukarimu, burudani na matukio ya jiji lote la Dubai, kwa kuzingatia burudani, usafiri wa familia, elimu na utalii wa matibabu.

Familia moja katika Textile Souk.
Image: HISANI

Idara ya Uchumi na Utalii ya Dubai (DET) katika muendelezo wa shughuli zake zinazoendelea barani Afrika imetoa tarehe za maonyesho yake ya barabarani katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Baada ya maonyesho yaliyofana nchini Nigeria na Afrika Kusini, DET imehitimisha mipango ya kuandaa awamu nyingine ya maonyesho nchini Ethiopia, Uganda na Kenya. Maonyesho ya Kenya yatafanyika Septemba 22.

Maonyesho hayo yataangazia ziara za bei nafuu jijini Dubai na huduma zingine  jiji hilo kwa washirika wake muhimu wa usafiri katika miji inayolengwa.

Vivutio vya onyesho hayo ni katika sekta za safari, ukarimu, burudani na matukio ya jiji lote la Dubai, kwa kuzingatia burudani, usafiri wa familia, elimu na utalii wa matibabu.

Mambo muhimu ya hafla hiyo ni pamoja na vipindi vifupi vya  ushirikiano, mawasilisho ya washirika, mikutano ya ana kwa ana, na taarifa kutoka vituo vya matibabu.

Takwimu mpya za utalii kutoka DET zinaonyesha kuwa kwa ujumla, hoteli za Dubai zilidumisha kiwango cha wastani cha upangaji wa asilimia 76 kuanzia Januari hadi Mei 2022.

Familia ya Kiafrika huko Abra.
Image: HISANI

Kulingana na takwimu kutoka kwa kampuni ya uchanganuzi ya usimamizi wa hoteli ya STR, Dubai iliorodheshwa nambari moja ulimwenguni katika umiliki wa hoteli, mbele ya maeneo mengine ya kimataifa ikiwa ni pamoja na New York (asilimia 61), London (asilimia 60) na Paris (asilimia 57), kwa Januari. -Aprili 2022 kipindi.

Baadhi ya mashirika yatakayoambatana na DET kwenye Roadshow ni pamoja na Hoteli, Hospitali, Vivutio, Makampuni ya Usimamizi wa Maeneo na wadau wengine katika mfumo wa ikolojia ya Utalii wa Dubai.

Meneja Msaidizi, Uhusiano wa Kimataifa (Afrika) kwa Utalii wa Dubai (DET) Tareq Binbrek alisema Afrika Mashariki ni soko kubwa la Utalii wa Dubai na ni nyumbani idadi kubwa ya safari zetu kutoka Afrika.

"Hili ni Roadshow ya kwanza baada ya janga na tuna furaha kurejea. Tunatazamia kufanya kazi kwa karibu na washirika wetu wa kibiashara na kuzungumza moja kwa moja na watazamaji wetu. Mambo mengi mapya na ya kusisimua yametokea Dubai tangu ziara yetu ya mwisho. kwa ukanda huu, kwa hivyo tunatarajia kushiriki habari njema na wasafiri wetu wote wa Afrika Mashariki,” alisema.

(Utafsiri: Samuel Maina)