- Alisema kuwa wameanzisha zoezi la kufuatilia mashambulizi ya Turkana kama walivyofanya kwa mashambulizi ya Mpeketoni na Kapedo
Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) imelaani shambulio la ujambazi la Turkana lililosababisha vifo vya maafisa 10 wa utawala na raia siku ya Jumamosi.
Shambulizi hilo lilitokea katika Kijiji cha Namariat katika Kaunti ya Turkana.
Katika taarifa siku ya Jumatatu, mwenyekiti wa IPOA Anne Makori alisema watafuatilia na kutoa mapendekezo kuhusu shambulio hilo.
"Kwa nchi yoyote, kupoteza maafisa wa usalama na wananchi kupitia vitendo vya uhalifu ni suala la kutia wasiwasi mkubwa," Makori alisema.
IPOA condemns and launches a monitoring exercise to establish the circumstances around the attack on eleven people in Namariat village including the dedicated officers who were carrying out their duties. ^FN pic.twitter.com/XVbI6NFTXY
— IPOA (@IPOA_KE) September 26, 2022
"Ni matumaini yetu kwamba kutakuwa na hatua madhubuti za uongozi wa polisi kulingana na uzito wa uhalifu uliofanyika katika kijiji cha Namariat."
Alisema kuwa wameanzisha zoezi la kufuatilia mashambulizi ya Turkana kama walivyofanya kwa mashambulizi ya Mpeketoni na Kapedo.
Zoezi la ufuatiliaji litaongozwa na Kurugenzi ya Ukaguzi, Utafiti na Ufuatiliaji ili kubaini mazingira ya shambulio la Turkana.
Makori alisema iwapo ufuatiliaji huo utatekelezwa kikamilifu, utasaidia katika kupunguza changamoto za usalama nchini Kenya.
"Hii ni sawa na kupinga mamlaka ya Kenya na inataka jibu thabiti lakini halali la polisi ili kuhakikisha amani idumu kote nchini," Makori alisema.