Wahindi waliotoweka ni wanadamu, walistahili kuishi - Raila Odinga

Tunatumai kwamba watapatikana wakiwa hai na kwamba haki itatendeka katika kesi yao. - Odinga.

Muhtasari

• Lakini pia tunaamini raia hao wa India si wa kwanza kutoweka na pia huenda hawatakuwa wa mwisho kama matukio ya awali ni kitu cha kutumia kama kigezo - Odinga.

Odinga azungumzia Wahindi waliotoweka
Odinga azungumzia Wahindi waliotoweka
Image: Facebook

Kinara wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga kwa mara ya kwanza amevunja kimya kuhusu kuhojiwa kunaoendelea kwa baadhi ya waliokuwa maafisa wa kitengo klichovunjiliwa mbali na rais Ruto cha SSU.

Odinga akizungumza mchana wa Alhamisi katika mkutano na vyombo vya habari alisema kwamba rais Ruto anaonekana kutaka kulipiza kisasi kutokana na kutoweka kwa rais wawili wa India ambao walikuwa wandani wake kabla ya kupotea kwa njia za utatanishi mwezi Julai mwaka huu.

Kinara huyo alisema kwamba rais Ruto anatumia nguvu nyingi sana kutaka kujua rais hao walienda wapi huku akiwahukumu baadhi ya maafisa wanaohusishwa na kutoweka kwao, jambo ambalo linaonekana kuegemea upande mmoja kisheria.

Aidha, Odinga alisema kwamab hakuna mtu angependa kuona mtu wa familia yake akitoweka na kusema kila mtu anaomba rais hao wa India na dereva wao Mkenya watapatikana wakiwa salama salimini.

Odinga vile vile aliinyooshea serikali ya Ruto kidole cha lawama kwa kusema kwamba rais hao wa India sio wa kwanza kutoweka na pia kusema kama mambo kadhaa hayatabadilishwa kwenda mbele basi watu wengi tu watazidi kutoweka na raia hao wa India hawatakuwa wa mwisho.

“Ruto anaonekana kuwatafuta baadhi ya Wahindi aliowapoteza katikati ya uchaguzi wa Agosti. Wahindi hao walikuwa wanadamu. Walistahili kuishi na tunaendelea kuombea familia zao na tunatumai kwamba watapatikana wakiwa hai na kwamba haki itatendeka katika kesi yao. Lakini pia tunaamini raia hao wa India si wa kwanza kutoweka na pia huenda hawatakuwa wa mwisho kama matukio ya awali ni kitu cha kutumia kama kigezo,” Odinga alisema.