Familia yalilia serikali kuchuguza upya kutoweka kwa mchekeshaji wa kikuyu 'Kianangi' aliyetoweka miaka 5

Kianangi aliondoka kwenda kumtembelea mamake aliyekuwa mgonjwa lakini hakurejea nyumbani miaka mitano sasa.

Muhtasari

• Septembe 21, 2007 Mwangi mwenye umri wa miaka 40 aliondoka nyumbani kwake mtaani Kasarani mwendo wa saa nne unusu mchana.

• Hakufika alikokuwa ameenda kumwona mamake aliyekuwa mgonjwa.

Mchekeshaji wa kikuyu Geoffrey Mwangi almaarufu Kianangi.
Mchekeshaji wa kikuyu Geoffrey Mwangi almaarufu Kianangi.
Image: Facebook

Mkewe mchekeshaji maarufu wa kikuyu Geoffrey Mwangi almaarufu Kianangi anaiomba serikali kumsaidia kumtafuta mumewe aliyetoweka kwa njia tatanishi miaka 5 iliyopita.

 Catherine Njeri, alitoa wito kwa Rais William Ruto na Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki kumsaidia kuanzisha tena juhudi zakumtafuta Mwangi.

Mama huyo alisema  mumewe aliondoka kwenda kumtembelea mamake aliyekuwa mgonjwa  lakini hakurejea nyumbani miaka mitano sasa.

Mnamo Septembe 21, 2007 Mwangi mwenye umri wa miaka 40 aliondoka nyumbani kwake mtaani Kasarani mwendo wa saa nne unusu mchana.

Njeri alisema walizungumza na mumewe kwa simu akiwa njiani kwenda kumuona mamake  wakati ambapo Mwangi alimpigia na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kuzungumza naye. 

Familia ilifichua kwamba iliandikisha taarifa katika kituo cha Polisi cha Ruiru mnamo Septemba 21, 2017 baada ya kumtafuta Mwangi hospitalini na makafani ya Kiambu, Embu, Kirinyaga, Nairobi, Murang’a, Machakos na Kajiado bila mafanikio wala dalili za kumpata.

Mwangi alianza kupata umaarufu tangu mwaka wa 2013 katika maeneo ya Mlima Kenya wakishirikiana na mwingizaji mwenzake mwenye jina Ephantus Mbuthia almaarufu Macang’i alipoanzisha tasnia yake ya kuwatumbuiza kwa vichekesho kwa lugha ya Kikuyu.