Wanawake 2 wakamatwa wakiwa na watoto wachanga waliokufa

Aliongeza kuwa wananchi wameona jambo lisilo la kawaida kwa wawili hao na hivyo kutoa taarifa kwa Nyumba Kumi.

Muhtasari
  • Kulingana na afisa wa Nyumba Kumi Paul Kirui, wawili hao ambao walinaswa ndani ya nyumba yao ya kukodisha walishukiwa kuwa walitoa mimba Jumanne usiku
Pingu
Image: Radio Jambo

Wakaazi wa kituo cha biashara cha Chepseon huko Kipkelion Mashariki, Kaunti ya Kericho, Alhamisi walipatwa na mshtuko baada ya wanawake wawili wa umri wa makamo kukamatwa wakiwa na watoto wachanga waliokufa.

Kulingana na afisa wa Nyumba Kumi Paul Kirui, wawili hao ambao walinaswa ndani ya nyumba yao ya kukodisha walishukiwa kuwa walitoa mimba Jumanne usiku.

Bw Kirui alisema mmoja wa wanawake hao ambaye alikuwa mmiliki wa nyumba ya kupanga, alifunga kijusi chake kilichokufa kinachoaminika kuwa na umri wa miezi saba na nguo kuukuu na kukiweka kwenye mkoba wake.

Mwanamke mwingine, kwa upande mwingine inasemekana alitupa chake kwenyeshimo la choo.

Kulingana na ripoti ya Citizen Digital,Bw.Kirui alisema wanawake hao waliwapa maafisa wa Nyumba Kumi taarifa zinazokinzana, jambo ambalo liliwatia shaka na kuwafanya waitishe mahojiano zaidi.

Aliongeza kuwa wananchi wameona jambo lisilo la kawaida kwa wawili hao na hivyo kutoa taarifa kwa Nyumba Kumi.

Kulingana na  Kirui, baada ya kuhojiwa zaidi, mwanamke aliyekuwa mwenyeji alikiri baadaye kwamba alitoa mimba na kutupa kijusi hicho cha miezi 5 ndani ya shimo la choo.

Maafisa kutoka Kituo cha Polisi cha Chepseon waliarifiwa na kukimbizwa katika eneo la tukio, wakatoa vijusi na kuwapeleka katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya kaunti ndogo ya Londiani.

Kisha wanawake hao walipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Londiani ambako walizuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani.