Mwanaume akamatwa kwa kujitoma bwenini na kondomu kwa lengo la kushiriki mapenzi na wanafunzi wa kike

Mkuu wa shule na mlinzi walivutiwa na zogo hilo na kukimbilia eneo la tukio kwa haraka.

Muhtasari
  • Akiwa ameshtushwa na hali hiyo, mwanaume huyo alitoka kwa kasi, lakini haikuchukua muda mlinzi wa shule alimkamata
Pingu
Image: Radio Jambo

Mwanamume mmoja alikamatwa baada ya kunyemelea bweni la wasichana kaunti ya Nyeri akiwa na dhamira ya kukutana na mpenzi wa maisha.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 18 kutoka shule ya kutwa ya Gatugi huko Karima alikuwa akijaribu kumtafuta mpenzi wake kutoka kwa umati wa wasichana wengine.

Hata hivyo, jitihada zake hazikuzaa matunda kwani aliibua shaka, na wasichana hao wakagundua kuwa walikuwa wakizungumza na mwanamume na si mwanafunzi mwenzao kama walivyofikiri hapo awali.

Mkuu wa shule na mlinzi walivutiwa na zogo hilo na kukimbilia eneo la tukio kwa haraka.

"Misheni ya kijana kukutana na mpenzi wake katika shule ya upili katika kaunti ya Nyeri jana usiku, iliambulia patupu baada ya mwanamume huyo wa miaka 18 kufichuliwa na wasichana wengine ambao walipaza sauti.

Maafisa wa polisi waliarifiwa na mkuu wa shule na walijibu mara moja. Kijana huyo aliwaambia maafisa hao kwamba alikuwa amealikwa na mpenzi wake kwa ajili ya biashara fulani ambayo haijatajwa, ambayo maafisa hao hawakuweza kuthibitisha mara moja,"DCI Ilisema.

Kulingana na duru za habari  mvulana  huyo alikuwa amevalia sare za shule ya msichana kutoka juu hadi chini huku akiungana na wasichana wengine kutoka kwa maandalizi yao ya jioni kukimbilia mabweni yaosaa nne usiku.

Mwanamume huyo alikuwa amejihami na pakiti za kondomu, ambazo alipaswa kuzitumia usiku kukidhi mahitaji yake.

Akiwa ameshtushwa na hali hiyo, mwanaume huyo alitoka kwa kasi, lakini haikuchukua muda mlinzi wa shule alimkamata.

"Hata hivyo, kondomu tatu, simu ya mkononi zilipatikana kutoka kwa mwanafunzi huyo mwenye bidii sana ambaye alikuwa amejaza vipande vya nguo kifuani mwake, ili kuzua taswira ya uwongo ya mwanafunzi huyo, Alisafirishwa hadi kituo cha polisi cha Othaya ambako anashughulikiwa."