logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanawake 3 wafariki kwa kuporomokewa na ukuta wakichimba dhahabu mgodini

Kutokana na ripoti ya Citizen Digital, watatu hao waliokuwa kati ya umri wa 20 hadi 32

image
na Radio Jambo

Michezo23 November 2022 - 06:38

Muhtasari


• Shughuli za uokoaji zikiongozwa na Karotich akisaidiwa na wakaazi waliofika upesi walisaidia katika uokoaji na kufanikiwa kutoa miili ya watu.

3 wafariki wakichimba dhahabu Pokot Magharibi.

Wakaazi wa eneo la Nyelnyel huko Pokot Magharibi wamegutushwa na kifo cha wanawake 3 waliokufa kutokana na kuta za mgodi waliokuwa wakichimba madini asubuhi ya kuamkia Jumatatu.

Kutokana na ripoti ya Citizen Digital, watatu hao waliokuwa kati ya umri wa 20 hadi 32  waliporomokewa na walikuwa wanajaribu kuchimba madini, tukio lililowaacha wawili kuumia.

Naibu wa chifu wa eneo hilo Flomena Karotich alisema walikuwa wameenda  kuchimba dhahabu kwenye mgodi huo wakati kuta zilipoporomoka na kuwazika wakiwa hai.

Shughuli za uokoaji ziliongozwa na Karotich akisaidiwa na wakaazi waliofika upesi walisaidia katika uokoaji na kufanikiwa kutoa miili ya watu hao mwendo wa saa moja asubuhi na miili yao kufikishwa katika makafani ya Kapenguria na waliojeruhiwa wakiendelea kupata nafuu kwenye hospitali ya Sigor.  

Naibu chifu mbali na hayo aliwaomba wakaazi wajitafutie njia zingine mbadala ya kujitafutia chakula, badala ya kuingia katika shughuli za kuchimba madini inayoiweka maisha yao kwenye hatari.

Hata hivyo, Karotich amewataka wakazi wa eneo hilo kutafuta fursa nyingine za biashara na kuachana na uchimbaji migodi, akitaja hatari inayoletwa na maisha ya binadamu.

Haya yanajiri baada ya miezi kadhaa, wengine wanne kuripotiwa kuuawa katika vita vya kudhibiti eneo la uchimbaji dhahabu huko eneo la Isiolo. Mapigano yaliwaacha watano wakiwa na majeraha makali.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved