Watu 6 wafariki kwenye ajali ya barabarani Eldoret

Watu 6 walifariki akiwemo mtoto mchanga na kuwaacha waliojeruhiwa kukimbizwa hospitalini.

Muhtasari

• Watu wengine kadhaa waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi kwa matibabu.

Watu 6 wafariki kwenye ajali ya barabarani eneo la Kaptingo, Eldoret.
Watu 6 wafariki kwenye ajali ya barabarani eneo la Kaptingo, Eldoret.
Image: Facebook

Usiku wa Jumatano ya Novemba 23 wakaaazi wa Eldoret eneo la Kaptingo waligutushwa na ajali ya barabarani iliyowaacha watu sita wamefariki akiwemo mtoto mdogo.

Ajali hiyo liyohusisha magari 3 aina ya Isuzu Mux, matatu na trekta linaripotiwa kuwa dereva wa trekta hilo ambalo haikuwa na taa, alikuwa akisafiri kwa mwendo wa kasi huku akijaribu kuingia barabara Kuu.

Matatu iliyokuwa ikielekea Kitale kutoka Nairobi iliigonga trekta hilo huku Mux ambayo ilikuwa  nyuma ya PSV nayo ikaigonga gari hilo kutoka nyuma.

Kulingana na Kamanda wa polisi wa eneo hilo la Uasin Gishu Ayub Gitonga, madereva wa matatu na Mux ni miongoni mwa waathiriwa waliofariki papo hapo.

Majeruhi walipelekwa katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi kwa matibabu huku mabaki ya magari hayo yakikokotwa hadi Kituo cha polisi cha Yamumbi.

Haya yanajiri baada ya ripoti ya NTSA ya hivi majuzi kuripoti kuwa watu 4,103 wamekufa kwenye kati ya ajali 18,474 zilizoripotiwa hadi Novemba mwaka huu.

Kulingana na Meneja wa NTSA wa Nyanza bwana Aden Adow idadi ya waliofariki ni ya kutisha na kwamba kila mmoja nchini Kenya anapaswa kuchukua hatua ya kukomesha ajali nyingi za barabarani kwa kutii sheria za barabarani haswa msimu tunaoelekea wa Krismasi.

 "Tunawahimiza watumiaji wa barabara kutii sheria za trafiki kila wakati." Adow alisema.