logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Genge lavamia chumba cha kuhifadhi maiti, laharibu magari ya kubeba maiti

Mshukiwa mkuu ni  mtoto wa mumiliki wa shamba ambamo makafani hiyo imejengwa.

image
na Radio Jambo

Habari29 November 2022 - 10:21

Muhtasari


• Wezi hao walivamia chumba cha kuhifadhi maiti cha  Yatta iliyoko kaunti ya Machakos na kufanya uharibifu.

• Inaripotiwa kuwa genge hilo lilikuwa limelipwa kutekeleza ubinadamu huo.

Chumba cha kuhifadhi maiti

Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 30 ametiwa mbaroni na polisi kwa madai ya kuvamia chumba cha kuhifadhi maiti cha Yatta akiwa na wenzake siku ya Jumapili.

Mshukiwa mkuu ni  mtoto wa mumiliki wa shamba ambamo makafani hiyo imejengwa.

Kulingana na Kamanda wa polisi wa Yatta, Bernard Rono genge hilo liliigia ndani ya makafani na kuwadunga kisu maiti kabla kuharibu gari la kubebea maiti.

Mmiliki wa makafani hiyo Gideon Mule ambaye alishtushwa na kitendo hicho alimshutumu mwenye ardhi hiyo kwa kutotii agizo la mahakama kulipa shilingi milioni 7.

Mule alisema kuwa mwenye shamba alikuwa amekodi majambazi hao na kuwataka wamfurushe kabla hajafidiwa.

 "Anataka niondoke, ilhali mahakama ilieleza kwa kinaga ubaga kuwa anilipe shilingi milioni 7  ndio nihame. sasa amefanya vitisho na mashambulizi," Bwana Mule alisema.

Mule aliongeza kuwa genge hilo liliharibu magari ya kubebea maiti, huku maiti moja ikiharibiwa kabisa.

“Vioo vya magari ya kubebea maiti vilivunjwa na mwili mmoja uliharibiwa kabisa hata familia ya marehemu inahangaika,” Mule alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved