logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tulienda mafichoni kwa siku 3 baada ya drama ya Bomas-Guliye afichua haya

"Tulitazama Televisheni ili tu kuangalia ikiwa mnauana au mnasherehekea," alisema.

image
na Radio Jambo

Habari16 January 2023 - 10:43

Muhtasari


  • Guliye alisema mawasiliano pekee ambayo watatu hao walikuwa nayo kwa Wakenya na ulimwengu ilikuwa Televisheni

Kamishna wa IEBC Abdi Guliye amefichua kuwa walijificha kwa siku tatu kufuatia drama ya Bomas of Kenya ya Agosti 2022.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya baada ya uchaguzi wa 2022 Safari Park jijini Nairobi, Guliye alisema pamoja na Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo Marjan Marjan na Kamishna Boya Molu walijificha mahali pasipojulikana.

"Baada ya tangazo la Bomas la matokeo ya urais, nakumbuka tulienda Siberia katika kaunti yangu mwenyewe pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Marjan na kamishna Molu, tulijificha, tukazima simu na kuwaacha Bomas," alisema.

Kamishna huyo alisema ilibidi waondoe walinzi wao, wakaondoka Bomas na kupanda gari aina ya Toyota Noah.

Guliye alisema mawasiliano pekee ambayo watatu hao walikuwa nayo kwa Wakenya na ulimwengu ilikuwa Televisheni.

"Tulitazama Televisheni ili tu kuangalia ikiwa mnauana au mnasherehekea," alisema.

"Baada ya siku tatu za kujificha, tuligundua kuwa Wakenya walikuwa wameendelea na maisha, na tukasema hatuwezi kujificha tena."

Guliye pia alishukuru kwaya ya Bomas ambayo ililetea nchi burudani wakati wa drama hiyo.

"Unakumbuka drama ya Bomas, napenda kuwashukuru kwaya ya Bomas, hata vitu vilipokuwa vikiruka kushoto, kulia na katikati, baadhi ya vitu hivyo vilijeruhiwa kimwili, kwaya iliendelea kuimba, napenda kuwashukuru kwa hilo," sema.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved