Mke wa mwanamume aliyezama kwenye bwawa afichua mazungumzo yao ya mwisho

Kiiru anadai kuwa baada ya mazungumzo yao ya hivi majuzi, simu ya Maina iliita na hakuweza kupokea.

Muhtasari
  • Kiiru anadai kuwa baada ya mazungumzo yao ya hivi majuzi, alimpigia mumewe simu na hakuweza kupokea
Image: KWA HISANI

Mke wa mwanamume aliyeangamia baada ya gari lake kutumbukia kwenye bwawa la maji huko Juja, wilaya ya Titanic kaunti ya Kiambu, hatimaye amezungumza kufuatia mkasa huo Jumatatu usiku.

Kulingana na Citizen Digital Margaret Kiiru alidai kuwa mumewe Titus Maina alikuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa ambaye aliishi maisha kwa kuuza vifaa vya kiufundi.

"Siku ya Jumatatu asubuhi, mume wangu aliondoka kwenda kazini, na tulizungumza jioni karibu saa 7. Mara ya mwisho tulipozungumza, alisema alikuwa Juja kwa mkutano wa biashara, nilimuuliza kuhusu upendeleo wake wa chakula cha jioni, na ndivyo ilivyokuwa." Alisema.

Kiiru anadai kuwa baada ya mazungumzo yao ya hivi majuzi, alimpigia mumewe simu na hakuweza kupokea.

"Nilimpigia simu na kumtumia ujumbe lakini hakupatikana, jambo lisilo la kawaida kwake kwa sababu amekuwa akipatikana kila mara."

Kulingana na Kiiru, hakujua kuhusu kifo cha mumewe hadi alipopokea simu kutoka kwa rafiki yake mnamo Jumanne mwendo wa saa nane jioni, akimwambia aende katika kituo cha polisi cha Kimbo.

Kiiru akizungumzia mwanamke aliye kufa maji na mumewe alisema;

"Ingawa simfahamu, naamini mwanamke ambaye alikuwa na mume wangu usiku huo alikuwa rafiki, alikuwa na marafiki wengi kwa sababu ya aina ya biashara yake," alisema.