Mudavadi asema hajakataa kuhamia katika ofisi aliyopewa kwenye makao makuu ya reli

Imepita zaidi ya miezi miwili tangu Mudavadi ateuliwe kwenye wadhifa huo, hata hivyo bado hajahamia afisi hizo.

Muhtasari
  • Amri ya utendaji iliyotolewa Oktoba mwaka jana na Rais ilionyesha kwamba afisi ya katibu mkuu wa Baraza la Mawaziri itakuwa makao yake katika Makao Makuu ya Shirika la Reli la Kenya
Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi akihutubia wanahabari mjini Nairobi mnamo 19/01/2023 Picha: ANDREW KASUKU
Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi akihutubia wanahabari mjini Nairobi mnamo 19/01/2023 Picha: ANDREW KASUKU

Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi amekanusha madai kwamba alikataa kuhamia afisi zake katika jengo la makao makuu ya Railways.

Mudavadi alisema anaenda kuhamia jengo hilo mwezi Machi kwani ukarabati wa baadhi ya sehemu za kituo hicho unaendelea hivi sasa.

Sijakataa kuhamia kwenye jengo. Watu lazima waelewe kwamba kuna ukarabati, ambao unafanywa kwa sasa. Tunatumai yatahitimishwa kufikia katikati ya Machi kabla hatujahamia,” alisema Mudavadi wakati wa mahojiano Alhamisi.

Akitetea eneo la jengo hilo, Mudavadi alisema lipo ndani ya mtaa na ukaribu wa ofisi nyingine za serikali kinyume na taarifa kuwa ‘amesukumwa’ hadi eneo lenye kelele.

Amri ya utendaji iliyotolewa Oktoba mwaka jana na Rais ilionyesha kwamba afisi ya katibu mkuu wa Baraza la Mawaziri itakuwa makao yake katika Makao Makuu ya Shirika la Reli la Kenya.

Imepita zaidi ya miezi miwili tangu Mudavadi ateuliwe kwenye wadhifa huo, hata hivyo bado hajahamia afisi hizo.