'Sponsors' watawapotosha-Dorcas Gachagua kwa vijana

Alizungumza alipohudhuria hafla ya mtoto wa kiume katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Muhtasari
  • Dorcas alionya dhidi ya kitendo hicho ambacho kimeonekana kuwa ‘trend’ hasa kwenye mitandao ya kijamii
Mama Dorcas Gachagua
Mama Dorcas Gachagua
Image: Facebook

Kuchumbiana na wanaume wazee na wanawake wazee kutakuvunja moyo, Mke wa naibu Rais Gachagua Dorcas Gachagua amewaonya vijana.

Dorcas alionya dhidi ya kitendo hicho ambacho kimeonekana kuwa ‘trend’ hasa kwenye mitandao ya kijamii

"Sijui kama jina 'mama' au 'mubaba' linakupigia kengele, nakuomba kama mama, uwe mwangalifu," Alizungumza Dorcas.

Alizungumza alipohudhuria hafla ya mtoto wa kiume katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Dorcas  alisema chaguo la mwenzi linaweza kumfanya au kumvunja mtu mdogo.

"Shinikizo la mitandao ya kijamii kando na 'mubaba' na 'mumama' linaharibu wanafunzi wetu sio tu UoN bali ni jambo la kitaifa," alisema.

Wawili hao ni majina ya mitaani kuelezea mtu mzee ambaye yuko kwenye uhusiano na kijana. Dorcas aliwaonya wanafunzi wa UoN kutokana na kuzuru mtaa mmoja mjini ambao alisema una ‘shughuli za samaki.’

“Mungu atusaidie. Labda wao ni wageni kwako lakini mimi si mgeni katika jiji hili,” alisema.