Anapaswa kwenda jela-Herman Manyora ajibu madai ya mdibiti wa Bajeti Nyakango

Katika taarifa yake Mchambuzi huyo amesema hilo ni jambo ambalo hata karani wa akaunti hawezi kulifanya.

Muhtasari
  • Imefichuliwa kuwa baadhi ya watu ambao majina yao hayajatajwa walijaribu kumshawishi Margaret Nyakango kuondoa jumla ya sh bilioni 15

Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa Herman Manyora amejibu Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakango baada ya kufichua yaliyotokea siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu 2022.

Imefichuliwa kuwa baadhi ya watu ambao majina yao hayajatajwa walijaribu kumshawishi Margaret Nyakango kuondoa jumla ya sh bilioni 15 kutoka serikalini kwa siku 15 hadi Uchaguzi Mkuu.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Herman Manyora amesema kwa hiyo Margaret Nyakango aende jela na amehoji ni kwa namna gani angetoa fedha hizo kutoka kwa serikali kwa kutumia jumbe za Whats App.

Katika taarifa yake Mchambuzi huyo amesema hilo ni jambo ambalo hata karani wa akaunti hawezi kulifanya.

"Anafaa kwenda jela. Atawezaje kutoa pesa zetu kwa msingi wa Ujumbe wa What's App? Hata karani wa akaunti hawezi kufanya hivyo", ilisema taarifa ya Mchambuzi wa Kisiasa Herman Manyora.