Matiang'i azuiliwa kwa saa 5 baada ya dakika 15 za kuhojiwa - Otiende Amollo

Otiende Amollo, mbunge wa Rarieda amedai kuwa kuna mpango wa kulipiza kisasi kwa aliyekuwa katibu mkuu wa baraza la mawaziri

Muhtasari
  • "Nyakati za Kuvutia, Nikiwa na aliyekuwa katibu wa wizara ya Mambo ya Ndani Fred Matiangi Katika Makao Makuu ya DCI Kiambu.
Image: OTIENDE AMOLLO/TWITTER

Mbunge wa eneo bunge la Rarieda katika bunge la kitaifa Mhe Otiende Amollo ni miongoni mwa mawakili walioandamana na aliyekuwa katibu wa wizara ya mambo ya ndani Dkt Fred Matiang'i kuzuru katika makau makuu ya DCI.

Dkt Matiang'i anasakwa na wapelelezi hao kutokana na kile kinachodaiwa kueneza habari za uwongo kimakusudi kwamba maafisa wa polisi walikuwa wamezingira makazi yake Karen kaunti ya Nairobi.

Otiende Amollo, mbunge wa Rarieda amedai kuwa kuna mpango wa kulipiza kisasi kwa aliyekuwa katibu mkuu wa baraza la mawaziri licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama kuu.

Anasema kuwa bado wanazuiliwa na kwamba DCI inapanga kujihusisha na misheni yakulipiza kisasi.

Katika taarifa yake kwenye ukurasa wake wa twitter Otiende alisema;

"Nyakati za Kuvutia, Nikiwa na aliyekuwa katibu wa wizara ya Mambo ya Ndani Fred Matiangi Katika Makao Makuu ya DCI Kiambu. Saa 5 Baadaye, bado tumezuiliwa baada ya Dakika 15 Pekee ya maahojiano. , Licha ya Amri ya Mahakama Kuu! Huu Sio Upelelezi, Pure Vendetta & Witch-hunt. Inasikitisha Hakika," alisema.