Serikali inataka kumkamata Babu Owino na Mimi-Seneta Olekina adai

"Yuko wapi rafiki yangu @HEBabuOwino Naelewa wananifuatilia mimi na wewe,

Muhtasari
  • Madai yake seneta huyo yanajiri siku moja baada ya waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i kuhojiwa na DCI
LEDAMA 2
LEDAMA 2

Seneta wa Narok Ledama Olekina amedai kuwa serikali ya rais William Ruto inapanga kumkamata yeye na Babu Owino kabla ya maandamano kesho.

Olekina alisema ni wazi kwamba kuna kila aina ya majaribio ya serikali kumnyanyasa na kumdhalilisha kupitia mashtaka ya uwongo.

Vinginevyo, alitangaza kuwa yuko tayari kukamatwa.

"Yuko wapi rafiki yangu @HEBabuOwino Naelewa wananifuatilia mimi na wewe, wako busy kuandika taarifa za kutafuta mashtaka ya kukukamata wewe na mimi! Ngoja nishikilie maelezo yako niwaambie nipo tayari!"

Madai yake seneta huyo yanajiri siku moja baada ya waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i kuhojiwa na DCI.

Madai yake yalizua tafrani katika mtandao wa twitter na hizi hapa baadhi ya hisia za Wakenya;

es&es@Es: Mende anatisha lakini ni muoga ajabu. Mende anakimbianga tu.Ona amefunga barabara zote zalink na state hao. Anaogopa nini?? Ona Ruto amejiprotect yeye na jamii yake kwa pesa yako na yetu.While Amekuacha wewe na jamii yako ujitetee.ngaii

TMo: Can't wait for you two to be arrested and charged in a court of law

Lawrence Kioko: If you did nothing wrong you shouldn't be afraid

Victor Kenei: I thought uko n Rungu!! Na uchunge tu isifunjike kaa siku ile.

Kamau: You overrate yourself too much kiongozi. Maybe you are just guilty.