Ujumbe wa Ruto kwa Wakenya huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya wanawake

Alisema pia amejipanga kuondoa vikwazo vyote vinavyokwamisha maendeleo ya kufikia usawa wa kijinsia.

Muhtasari
  • Rais Ruto alikariri kujitolea kwa utawala wake kutimiza ahadi ya kujumuishwa kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi
RAIS WILLIAM RUTO
Image: TWITTER

Huku uimwengu ukiadhimisha siku ya wwanawake duniani, Rais William Ruto alikuwa na ujumbe kwa wanawake na Wakenya kwa jumla.

Katika ujumbe wake, Rais alisema anajivunia hatua iliyofikiwa na utawala wake katika kuhakikisha ushirikishwaji wa wanawake katika uongozi.

Rais Ruto alikariri kujitolea kwa utawala wake kutimiza ahadi ya kujumuishwa kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

"Hii ndiyo sababu nimeshiriki uongozi wa bunge kwa nia ya kuchukua hatua za pamoja za uzalendo wa pande mbili kutafuta njia ya kikatiba ya kukuza usawa na ushirikishwaji katika uwakilishi wa kisiasa," alisema.

Alisema pia amejipanga kuondoa vikwazo vyote vinavyokwamisha maendeleo ya kufikia usawa wa kijinsia.

Ruto alisema anategemea uungwaji mkono wa wanawake wa Kenya ili kufikia usawa wa kijinsia.

"Pia tunajitolea kuondoa vizuizi vya kimfumo na kusalia mkondo kuelekea usawa kwa wote nchini Kenya tukiwa na imani kwamba ushiriki kamili wa wanawake unaweza kutusaidia kutambua nusu inayokosekana ya bidhaa ya kitaifa ya nchi yetu. Heri ya Siku ya Wanawake."