logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DPP Haji afafanua ripoti zinazomhusisha Kalonzo katika kesi ya unyakuzi wa ardhi

Hapo awali, Makamu wa Rais wa zamani alitupilia mbali madai kama hayo

image
na Radio Jambo

Habari09 March 2023 - 12:00

Muhtasari


  • Akihutubia madai hayo mwaka wa 2021, Kiongozi wa Chama cha Wiper alitoa wito kwa mashirika ya uchunguzi kuchunguza na kusuluhisha suala hilo
  • Chapisho lililoenea kwenye mitandao ya kijamii likiwa na picha ya DPP Haji lilidai kuwa Kalonzo alikuwa anachunguzwa
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma mnamo Alhamisi, Machi 9, ilikanusha ripoti zinazodai kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji alikuwa amepokea ripoti ya kesi ya ardhi inayomkabili aliyekuwa makamu wa rais, Kalonzo Musyoka.

Katika taarifa, ODPP ilionyesha kuwa ripoti hizo ni ghushi na za kupotosha. Pia aliwataka wananchi kupuuza habari hiyo inaodaiwa kuwa imetoka ofisini kwake.

"ODPP ingependa kufahamisha umma kwamba taarifa kwenye bango lililoambatishwa ni ya kupotosha na si ya kweli," ilisoma taarifa hiyo.

Chapisho lililoenea kwenye mitandao ya kijamii likiwa na picha ya DPP Haji lilidai kuwa Kalonzo alikuwa anachunguzwa.

Kulingana na ripoti hizo bandia, DPP Haji alidai kuwa uchunguzi ulihitimishwa, na alikuwa akipokea ripoti ya mwisho.

“Nimepokea ripoti inayoelezea matokeo ya uchunguzi wa madai ya unyakuzi wa ardhi ya Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) na aliyekuwa Makamu wa Rais Mhe. Kalonzo Musyoka. Nitapitia faili na kushauri kuhusu hatua zinazofaa,” ilidai taarifa hiyo.

Hapo awali, Makamu wa Rais wa zamani alitupilia mbali madai kama hayo, akisema kwamba wapinzani wake walieneza kwa manufaa ya kisiasa.

Akihutubia madai hayo mwaka wa 2021, Kiongozi wa Chama cha Wiper alitoa wito kwa mashirika ya uchunguzi kuchunguza na kusuluhisha suala hilo la mara kwa mara kwenye sehemu ya ardhi.

Kalonzo alijiwasilisha kwa hiari yake mbele ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kuhojiwa ili kufuta jina lake kutokana na madai yanayohusu uwezekano wa mchakato usiofuata utaratibu wa kupata kipande cha ardhi huko Yatta kaunti ya Mahakos.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved