Niko tayari kwenda kuuza mandazi Kibera lakini Mau ihifadhiwe-Raila

Raila Odinga amewataka wafuasi wake kuendelea kusimama kidete dhidi ya serikali kwa manufaa yao.

Muhtasari
  • Alidai kuwa IEBC ilienda kinyume na katiba kwa kutangaza matokeo ya Kaunti ya Narok katika Bomas of Kenya badala ya katika makao makuu ya Kaunti hiyo
KINARA WA AZIMIO RAILA ODINGA
Image: RAILA ODINGA/TWITTER

Kiongozi mkuu wa Muungano wa Azimio Raila Odinga leo ameongoza wafuasi katika kaunti ya Narok kwa maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza.

Maandamano ya Raila Odinga yamehudhuriwa na idadi kubwa ya Wakenya wanaolalamikia gharama ya juu ya maisha katika utawala wa Kenya Kwanza.

Akihutubia umati, Raila Odinga ameeleza kuwa Msitu wa Mau unapaswa  kuhifadhiwa na yuko tayari kuuza Maandazi Kibera lakini ahakikishe kuwa Msitu wa Mau uko salama.

"Nilisema Mimi Niko tayari kwenda kuuza maandazi Kibera lakini Mau ihifadhiwe," Raila Odinga aliwaambia Wakenya wakati wa maandamano ya Azimio

Sasa pale Ruto anapiga kifua akija hapa anaongea mambo uongo lakini haamini Mau inawezahifadhiwa."

Raila Odinga amewaambia wakazi wa kaunti ya Narok kuwa yuko tayari kuwaongoza katika mwelekeo utakaokuwa na umuhimu mkubwa.

Raila Odinga amewataka wafuasi wake kuendelea kusimama kidete dhidi ya serikali kwa manufaa yao.

Raila alilaumu IEBC kwa kushindwa kwa Kenta kushinda kinyang'anyiro cha ugavana Narok.

Alidai kuwa IEBC ilienda kinyume na katiba kwa kutangaza matokeo ya Kaunti ya Narok katika Bomas of Kenya badala ya katika makao makuu ya Kaunti hiyo.

Raila alisema kuwa huo ndio uharamu anaoshughulikia kubadilisha.