Musalia Mudavadi amtembelea aliyekuwa naibu Rais Moody Awori

Muhtasari
  • Kulingana na Mudavadi, ilikuwa ishara nzuri kumpata kwa sababu walibadilishana masuala kadhaa ambayo viongozi wanapaswa kuzingatia katika nchi yetu.
Image: TWITTER

Mkuu wa Mawaziri  Musalia Mudavadi leo amemtembelea aliyekuwa Makamu wa Rais Moody Awori katika makazi yake Nairobi.

Kulingana na Mudavadi, ilikuwa ishara nzuri kumpata kwa sababu walibadilishana masuala kadhaa ambayo viongozi wanapaswa kuzingatia katika nchi yetu.

Mudavadi alimsifu kwa kuwa imara na shupavu.

"Ilikuwa ni ishara ya kupendeza kukutana naye tulipojadiliana kuhusu masuala kadhaa ambayo tunapaswa kuzingatia kama nchi; miongoni mwao hitaji la kukuza umoja na utangamano endelevu miongoni mwa Wakenya na kufanyia kazi utekelezaji wa manifesto ya Kenya Kwanza.

Sisi pia ilichukua muda kutafakari siku tulizohudumu pamoja serikalini. Katika umri wake, Mzee anabaki imara na shupavu." Aliandika Mudavadi.

Haya yanajiri siku chache baada ya makamu huyo wa zamani kukutana na Katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini Francis Atwoli, mwanasheria mkuu mstaafu na ambaye pia alikuwa seneta wa Busia Amos pamoja na aliyekuwa mbunge wa Westlands Fred Gumo