Tunahitaji vyoo safi wakati wa maandamno-Sifuna amwambia Sakaja

Raila alikuwa ametangaza kuanza kwa shughuli kubwa, na maandamano ya mitaani mnamo Machi 20.

Muhtasari
  • "Gavana Sakaja azingatie kuandaa Jiji kwa wageni wetu tarehe 20. Tunataka vyoo safi vya umma, maji ya kunywa katika CBD,
SENETA WA NAIROBI EDWIN SIFUNA
Image: TWITTER

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ametoa mataka kadhaa ya usalama kwa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja kuhusu maandamano yaliyopangwa na upinzani mnamo Machi 20.

Sifuna alimtaka Sakaja kuzingatia kuandaa jiji kwa wageni watakaoingia barabarani kutokana na gharama ya juu ya maisha na matakwa mengine kama alivyosema kinara wa ODM Raila Odinga.

"Gavana Sakaja azingatie kuandaa Jiji kwa wageni wetu tarehe 20. Tunataka vyoo safi vya umma, maji ya kunywa katika CBD, ambulensi zetu na vifaa vya matibabu kwenye hali ya kusubiri, wasimamizi wa trafiki kuongoza trafiki na kulinda wageni nk,"Aliandika Sifuna.

Raila alikuwa ametangaza kuanza kwa shughuli kubwa, na maandamano ya mitaani mnamo Machi 20.

Kiongozi huyo wa Azimio na timu yake walizindua mpango mpya uliopewa jina la Movement for Defense of Democracy, wakitoa makataa  15 kwa nini Ruto lazima ajiuzulu.

Baadhi ya masuala aliyoyataja ni pamoja na gharama ya juu ya maisha, kutozwa ushuru kupita kiasi, uingizaji wa GMO, uundaji upya wa IEBC unaoendelea, udanganyifu wa uchaguzi, kudhulumiwa kwa makamishna wanne wa IEBC, kushughulikia vibaya ombi la urais la Azimio na mahakama kuu miongoni mwa makataa mengine.