Mama Rachel Ruto amkaribisha Mama taifa wa Italia Laura Mattarella Kenya

Laura Mattarela aliandamana na babake ambaye ni Rais wa Italia.

Muhtasari

• Laura Mattarella, ambaye ni binti wa rais Sergio Mattarella, aliwasili nchini siku ya Jumatatu akiwa ameandamana na rais, Sergio.

Mama wa taifa Rachel Ruto, siku ya Jumanne alimkaribisha binti ya rais wa Italia Laura Mattarella nchini Kenya.

Laura Mattarella, ambaye ni binti wa rais Sergio Mattarella, aliwasili nchini siku ya Jumatatu akiwa ameandamana na rais, Sergio, katika ziara rasmi ya siku nne.

Bi  Ruto alimkaribisha Bi Matarella katika Ikulu ya Nairobi wakiwa na waziri wa Utalii Penina Malonza.

"Karibu Kenya Laura Mattarella,Mama taifa wa jamuhuri ya Italia." Bi Ruto alisema.

Baadaye wawili hao walifululiza hadi ukumbi wa Bomas ili kupata utamu wa mandhari ya  utamaduni wa watu wa Kenya na kuipa Kenya fursa kunadi tamaduni za Kenya nchini Italia. 

Wakiwa Bomas waliweza kuburudishwa kwa ngoma za kitamaduni za jamii mbali mbali.

Rais Sergio Matterela ni mjane, mke wake, Marissa Chiazesse, alifariki mwaka wa 2012.

Majukumu ya mama wa taifa yalitwaliwa yalipewa bintiye, Laura.